Maktaba ya Kila Siku: August 27, 2025

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu Kailima R.K, amefunga kikao cha siku mbili cha Tume na Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili kamili na ambavyo vimependekeza wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais. Kikao hicho kiliitishwa kwa lengo la kujadili na kupanga kwa pamoja ratiba ya kampeni za vyama hivyo

Kikao hicho kilichoketi Agosti 25 na 26, 2025 kilishirikisha vyama vya Civic United Front (CUF), National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha Mapinduzi (CCM), National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party …

Soma zaidi »