Leo Februari 23, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, iliyopo Mkata-Mbweni, mkoani Tanga. Hospitali hii inajumuisha majengo 15, ikiwa ni pamoja na wodi za wanawake, wanaume, na watoto, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, jengo la upasuaji, huduma za dharura (EMD), na mengineyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Omary Mchengerwa amesema Serikali kuu ilitoa kiasi cha Tshs. Bilioni 4.37 huku wadau wengine wa maendeleo wakichangia ujenzi wa majengo mengine ikihudumia Kata 21, Vijiji 91 na Vitongoji zaidi ya 700.
Hospitali imeanza kutoa huduma mbalimbali, zikiwemo za wagonjwa wa nje, dharura, kulaza wagonjwa, kliniki ya baba, mama na mtoto, chanjo, huduma za kujifungua na upasuaji, maabara, ultrasound, na huduma za kuhifadhi maiti.
#sisinitanzania #tanzaniayetu #samia #samianatanzania #tanzanianamaendeleo #tanzaniayetu #nchiyangu #sisinitanzaniamoja #sisinitanzania🇹🇿
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+