Tunawatakia Watanzania wote furaha, amani, na upendo katika kipindi hiki cha Noeli. Tuwe na muda wa kusherehekea pamoja na familia na marafiki, huku tukikumbuka maana halisi ya sikukuu hii—upendo, ukarimu, na mshikamano. Mungu aendelee kuibariki nchi yetu Tanzania na kutupa mwaka mpya uliojaa matumaini na mafanikio. Noeli Njema na Mwaka …
Soma zaidi »Maktaba ya Mwaka: 2024
Ujenzi wa Kituo cha Afya Igava, Kijiji cha Igunda Muungano, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Unaendelea kwa Kasi
Kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Igava kilichopo Kijiji cha Igunda Muungano, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, inaendelea kwa kasi. Ujenzi huu unafadhiliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 400, zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Fedha hizi ni …
Soma zaidi »Ushirikiano wa Wananchi na Serikali katika Kuboresha Huduma za Afya
Kituo cha Afya Kafita, kilichopo katika Wilaya ya Nyang’hwale, Kata ya Kafita, kijiji cha Kafita, ni mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya wananchi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), na serikali kuu. Ujenzi wa kituo hiki umegharimu jumla ya shilingi milioni 200, fedha ambazo zilitokana na juhudi za wananchi, …
Soma zaidi »NEMC YATOA ONYO SAUTI ZILIZOZIDI VIWANGO NA UTIRIRISHAJI WA MAJI TAKA MSIMU WA SIKUKUU
Shule ya Sekondari ya Geita Girls imekuwa miongoni mwa miradi muhimu ya serikali inayolenga kuboresha sekta ya elimu nchini Tanzania. Hadi sasa, ujenzi wa shule hii umegharimu takribani TZS bilioni 4.35. Shule hii imeanza kupokea wanafunzi, na tayari zaidi ya wanafunzi 100 wapo shuleni hapo wakijifunza katika mazingira bora na ya kisasa
Licha ya mafanikio haya, juhudi za ujenzi bado zinaendelea. Mabweni ya kisasa yamepangwa kujengwa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata sehemu salama za kuishi, na ukumbi wa mikutano unaendelea kujengwa kwa lengo la kuwapa wanafunzi na walimu nafasi ya kushiriki mikutano na shughuli mbalimbali za kitaaluma na kijamii. Kuimarisha Usawa wa Kijinsia …
Soma zaidi »Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 pamoja na barabara unganishi yenye urefu wa kilomita 2.3
Hafla hiyo ilifanyika katika mkoa wa Simiyu, ambapo Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ipo imara na imejidhatiti kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wote nchini. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Majaliwa aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi …
Soma zaidi »UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MWENDOKASI AWAMU YA NNE WAENDELEA KWA KASI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) awamu ya nne, ikiwa ni juhudi za kuboresha usafiri wa umma jijini Dar es Salaam. Awamu hii inahusisha ujenzi wa njia kuu ya mwendokasi yenye urefu wa kilometa 13.5, inayotoka …
Soma zaidi »HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA YAPATA USAFIRI KUWAFIKIA WANANCHI WENGI ZAIDI
Katika juhudi za kuhakikisha haki inawafikia wananchi wa kila kona ya Tanzania, huduma ya msaada wa kisheria sasa imeimarishwa kwa kupata usafiri wa kisasa. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kupanua wigo wa huduma za kisheria kwa wananchi wote, hususan wale wa maeneo ya vijijini na walio katika mazingira …
Soma zaidi »Ijumaa, Desemba 20, 2024, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi rasmi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara. Nyumba hizo zimejengwa katika kitongoji cha Waret, Hanang, ikiwa ni juhudi za Serikali kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika na kuimarisha ustawi wao
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapa pole waathirika wote na kusisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwasaidia. “Ujenzi huu ni ishara ya upendo na kujali kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, aliyetoa maelekezo ya kujenga nyumba bora na za kudumu kwa …
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 20, 2024 amezindua nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba mwaka jana katika kijiji cha Gendabi wilayani Hanang Mkoa wa Manyara
Pichani, Waziri Mkuu akizungumza na Brightina Francis wa kijiji cha Gendabi baada ya kuzindua nyumba hizo zilizojengwa katika kitongoji cha Waret wilayani humo
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+