RAIS SAMIA UFUNGUA KIWANDA CHA SARUJI NA CHOKAA PHASE TWO CHA MAWENI LIMESTONE LTD

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka historia kwa kufungua rasmi Kiwanda cha Saruji na Chokaa cha Maweni Limestone kilichopo Jijini Tanga. Uwekezaji huu mkubwa unalenga kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda nchini, sambamba na dhamira ya serikali ya kuirejesha Tanga katika hadhi yake kama kitovu cha viwanda Tanzania.

Rais Dkt. Samia amepongeza hatua ya Maweni Limestone kupanua uwekezaji wake nchini, akisema kuwa ni ishara ya kuimarika kwa mazingira ya biashara, usalama wa uwekezaji, na imani ya wawekezaji kwa sera za serikali. Ameeleza kuwa uwekezaji huu siyo tu unatoa fursa za ajira kwa Watanzania, bali pia unachangia katika upatikanaji wa malighafi muhimu kwa ujenzi, hivyo kusaidia miradi ya maendeleo nchini.

Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje kwa kuhakikisha kuwa kuna sera thabiti, miundombinu bora, na upatikanaji wa malighafi kwa urahisi. Pia, amepongeza jitihada za sekta binafsi katika kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya viwanda, ambayo inalenga kujenga uchumi imara na endelevu kwa Watanzania wote.

Meneja Rasilimali watu na Utawala Bwana Jackson Gerald Sumbi ameeleza kuwa kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi takribani 900.

Aidha, baadhi ya wananchi wamempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuweka mazingira bora yanayovutia wawekezaji katika viwanda, hata hivyo wameahidi kumchaguz tena katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025.

#DktSamiaTanga #sisinitanzania #ikulumawasiliano #Mpango #MSLAC

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *