Tarehe 26.02.2025
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga amegawa boti 35 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.47 kwa wavuvi wa Wilaya ya Pangani ikiwa ni awamu ya pili kwa Rais Mhe. Dkt. Samia kutoa boti kwa wavuvi Mkoani Tanga.
Boti hizo zina uwezo wa kubeba mzigo wa samaki wenye tani 3 hadi 4 na zimetoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuweza kujipatia vipato vya kujikimu.
Pia, Ugawaji wa boti hizo unaenda sambamba na utoaji wa mikopo isiyokuwa riba kwa wavuvi ili kuwawezesha kuziendesha boti kwa tija na kukuza mitaji yao.
@samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano #sisinitanzania #tanzaniayetu #tanga #tanzania #sisinitanzaniampya #maendeleo #DktSamianaTanga
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+