Maktaba ya Mwezi: November 2025

Tanzania:ukurasa mpya wa amani kwa kuzindua Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani

Dodoma, 20 Novemba 2025 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua rasmi Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. Tukio hilo lilikuwa …

Soma zaidi »

DKT. MWIGULU AKUTANA NA KATIBU MKUU WA TEC

Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 20, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Soma zaidi »

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo 20 Novemba, 2025, amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko kwenye ofisi za Wizara zilizoko mtumba mkoani Dodoma, na kumshukuru Mhe. Biteko kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake.

Waziri Ndejembi amesema katika kipindi cha uongozi wake, utendaji kwenye sekta ya nishati umekuwa kwa kiasi kikubwa na huduma za utendaji zimeboreshwa na tija kuonekana katika harakati za kukuza sekta ya nishati. Waziri Ndejembi ameahidi atayaendeleza yote pale alipoishia Mhe.Biteko, ili kuhakikisha azma ya serikali na maono iliyonayo kufanikisha miradi …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba muhimu mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya Ikulu. #RaisSamia #MawaziriWapya #Ikulu #HotubaYaRais #Tanzania

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AMEKABIDHIWA RASMI OFISI NA WAZIRI MKUU MSTAAFU KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alikabidhiwa rasmi ofisi na Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa Novemba 17, 2025, Mlimwa, Dodoma. Hafla ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Doto Biteko, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Soma zaidi »

SERIKALI IMEAHIDI KULIFANYIA KAZI SWALA LA MABADILIKO YA KATIBA – RAIS. DKT. SAMIA

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kulipa kipaumbele suala la mabadiliko ya Katiba na kwamba hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ili kufikia mwafaka unaokubalika kwa Watanzania wote. #kilimobiashara #tanzania #wakulima #fursazakilimo #africa #kilimobora #katibampya #KATIBAYATANZANIA #tanzania #samiasuluhu

Soma zaidi »

NAMWOMBA MWENYEZI MUNGU KUWA MWISHO WA AWAMU YA SITA USIPIMWE KWA VITU BALI KWA TABASAMU- RAIS SAMIA

“Namwomba Mwenyezi Mungu kuwa mwisho wa Awamu ya Sita usipimwe kwa vitu bali kwa tabasamu tutakaloliacha kwenye nyuso za Watanzania” — inatukumbusha maana ya uongozi unaogusa watu moja kwa moja. Ni wito wa kufanya kazi kwa moyo, kusikiliza wananchi na kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora zaidi kwa vitendo vinavyoonekana ndani …

Soma zaidi »

DKT. MWIGULU AAPISHWA IKULU CHAMWINO—RAIS SAMIA AELEZA SABABU ZA UTEUZI WAKE

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika hotuba yake, Rais Samia amesema uteuzi huo ulipitia ushindani mkubwa na Dkt. Mwigulu ndiye aliyebeba sifa nyingi zaidi kwenye vigezo vyote vilivyopimwa. Ameeleza kuwa majukumu ya Waziri Mkuu …

Soma zaidi »