“Tangu kuanza kwa mradi wa EACOP mwaka 2022 hadi sasa, jumla ya Watanzania 9,194 wamepata nafasi za kufanya kazi ndani ya mradi na hivyo kuwa fursa kwao ya kujipatia kipato, mwaka 2024 kampuni ilitoa mafunzo maalumu kwa Vijana 170 na kuwapatia kazi kwenye mradi, Vijana wengine 110 wapo katika masomo na wanatarajiwa kujumlishwa pia katika Mradi huo pamoja na kutoa ufadhili wa Vijana 238 katika vyuo mbalimbali nchini.”
Dkt. Biteko amesema hayo katika Kijiji cha Bukombe, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita tarehe 18 Agosti 2025 wakati akizindua mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+