DCEA YATUMIA NANENANE KUTOA ELIMU KWA JAMII NA KUHAMASISHA KILIMO CHA MAZAO MBADALA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeshiriki katika Maonesho ya Nanenane kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na kuwahamasisha kushiriki katika shughuli halali za uzalishaji mali, hususan kilimo, ufugaji na uvuvi.

Kamishina Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema ushiriki wa mamlaka hiyo unalenga kuunganisha agenda ya kilimo na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, akisisitiza kuwa wakulima wa bangi na mirungi wana nafasi ya kubadili maisha yao kwa kuachana na zao haramu na kujiunga katika vikundi vya kilimo halali.

Amefafanua kuwa vikundi hivyo vinaweza kunufaika na mikopo yenye riba nafuu kutoka taasisi za fedha pamoja na asilimia 10 ya mapato ya halmashauri, hatua itakayowawezesha kuanzisha miradi endelevu na kuboresha maisha yao.

Aidha, Kamishina Lyimo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo, hatua ambayo imewezesha fedha zaidi kufadhili miradi ya kilimo na kuhamasisha halmashauri kutoa mikopo kwa vijana ili kuanzisha mashamba na shughuli za ufugaji na uvuvi.

Katika maonesho hayo, DCEA pia imepata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali waliotembelea banda la mamlaka hiyo, na kuwahimiza kuepuka dawa za kulevya ili kufanikisha malengo yao ya kimasomo na maisha.

Kauli mbiu ya DCEA kwenye maonesho haya ni: “Kataa Dawa za Kulevya, Timiza Malengo.”

Unaweza kuangalia pia

🔴 LIVE: SAMIA SULUHU HASSAN AINGIA KWA KISHINDO MBEYA – MBALIZI

Rais Samia Suluhu Hassan amewasili Mbalizi, Mbeya, kwa kishindo kikubwa akipokelewa na umati wa wananchi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *