MRADI WA URANI WALETA AJIRA NA MATUMAINI KWA WAKAZI WA SONGEA SCOLASTICA

Bi. Scolastica Ernest Lole ni miongoni mwa wananchi walioguswa moja kwa moja na fursa za ajira kupitia mradi wa uchimbaji wa madini ya urani unaoendeshwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd. Akiwa mfanyakazi wa Ako Group Ltd kampuni iliyopewa zabuni ya kutoa huduma ya chakula, usafi wa mazingira na malazi ya wafanyakazi wa mradi huo, Scolastica anasema maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa.

Anasema kuwa kupitia mkataba wa Ako Group na Mantra, watu wengi kutoka vijiji vinavyozunguka mradi wamepata ajira za kudumu na za mkataba, hatua iliyosaidia kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza kipato kwa familia nyingi. Huduma wanazozitoa si tu zinawawezesha kiuchumi, bali pia zimejenga uzoefu wa kazi na taaluma mpya miongoni mwao.

Scolastica anaeleza kwa furaha kuwa uwepo wa mradi huu umekuwa baraka kwa wakazi wa Songea, kwani mbali na ajira, jamii imenufaika na huduma za kijamii kama maji, afya, na miundombinu bora. Anaamini kuwa huu ni mwanzo wa mabadiliko chanya ya kiuchumi kwa mikoa ya kusini na taifa kwa ujumla.

#UraniTz

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba muhimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *