Songea, Ruvuma – Katika mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji wa elimu ya kisheria na uwajibikaji kwa viongozi wa serikali za mitaa, mwanaharakati na mkazi mashuhuri wa Songea, Hamisi Abdala, ametoa kauli yenye uzito kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza mbele ya viongozi wa vijiji, kata na wananchi waliokusanyika katika semina ya mafunzo ya msaada wa kisheria, Hamisi Abdala aliwakumbusha Watanzania juu ya maneno ya kubeza yaliyotolewa na baadhi ya watu dhidi ya uwezo wa Rais Samia mwanzoni mwa utawala wake.
“Wapo waliodhani kuwa kwa sababu ni mwanamke, basi hatoweza. Walisema ni dhaifu, hataweza kutekeleza miradi mikubwa. Lakini leo hii, kila kona ya nchi kuna ujenzi, kuna barabara, kuna shule, kuna hospitali, kuna umeme vijijini. Tunasubiri nini kusema ukweli huu? Rais Samia ameweza, na Watanzania tuwe wa kweli tuuseme ukweli huu bila woga,” alisisitiza kwa msisitizo Hamisi Abdala huku akishangiliwa.
Katika hotuba hiyo ya hamasa, alitaja baadhi ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha takribani miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, ikiwa ni pamoja na:
Kukamilika kwa awamu mbalimbali za reli ya kisasa ya SGR, inayounganisha Dar es Salaam na maeneo ya ndani kwa kasi na ufanisi.
Ujenzi wa vituo vya afya na hospitali zaidi ya 300, zikiwemo hospitali za wilaya na za rufaa.
Mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajiwa kuzalisha megawati 2,115 – mafanikio ya kihistoria.
Upanuzi na ukamilishaji wa barabara za lami na madaraja makubwa kote nchini.
Elimu ya sekondari kuimarika kwa kujengwa kwa madarasa zaidi ya 18,000, na ongezeko la shule mpya za sayansi.
Hamisi Abdala amesisitiza kuwa wakati umefika sasa kwa kila Mtanzania kuachana na siasa za kubeza, na badala yake kuwa wakweli kwa yale ambayo yamefanyika. Amehimiza vijana, wanawake, na wazee kuwa mabalozi wa kusema ukweli kwa sauti juu ya maendeleo yaliyopo, akiamini kuwa “amani, maendeleo, na matumaini” ndio alama ya awamu ya sita.
“Tusiogope kusema: Rais wetu ameweza. Hii ni haki yake na ni wajibu wetu kusema ukweli huu. Taifa linaendelea. Tuunge mkono kwa vitendo.
” Ujumbe wa Hamisi Abdala umetafsiri hisia za wananchi wengi waliokuwa na shaka, lakini sasa wanashuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa ukiwapa huduma bora na matumaini mapya ya maisha.
#AwamuYaSita #SamiaSuluhuHassan #MiradiYaMaendeleo #TanzaniaInajengwa #MSLAC
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+