Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Chamwin

Tarehe 17 Mei, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Chamwino, iliyopo Kata na Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Afisa Mwandikishaji wa majimbo ya Chamwino na Mvumi Bw. Godfrey Mnyamale amewaomba wananchi wa Wilaya ya Chamwino kujitokeza kwa wingi kumsindikiza Rais Dkt. Samia na kutumia fursa hiyo kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwa wale ambao bado hawakufanya hivyo awamu ya kwanza.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari awamu ya pili litafanyika katika Mikoa 11 ya Tanzania Bara ambayo ni Dodoma, Manyara, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara huku likiendelea katika Mikoa ya Visiwa vya Pemba na Unguja.

Aidha, Wananchi kote nchini wamehimizwa kujitokeza mapema kwa kuwa zoezi hilo linatoa fursa ya siku saba pekee kuanzia tarehe 16 – 22 Mei, 2025

Vituo vya Uandikishaji vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12: 00 Jioni. Wananchi wakaoboresha taarifa zao na kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura watapata sifa za kushiriki Uchaguzi wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Unaweza kuangalia pia

“WAZEE NA WAZAZI WAACHE URITHI WA UZALENDO KWA VIJANA” – MHE, RAIS, DKT. SAMIA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *