TALGWU SINGIDA YAPONGEZA UAMUZI WA RAIS SAMIA KUFANIKISHA MEI MOSI KITAIFA

Katibu wa mkoa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) mkoa wa Singida, Deogratius Rugambwa, amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kufanyika kitaifa katika mkoa wa Singida.

Ameeleza kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria na inaongeza heshima kwa mkoa huo, huku ikileta hamasa kubwa kwa wafanyakazi na wakazi wa Singida.

Rugambwa amesema wafanyakazi wako tayari kwa ajili ya kumpokea na kumsikiliza Rais Samia katika siku hiyo muhimu.

Vilevile wafanyakazi wanatambua na kuthamini jitihada kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita, ikiwemo kupunguza kodi kwenye mishahara, kulipa madeni ya watumishi, na kuboresha huduma za afya kwa watumishi na wananchi kwa ujumla hasa kwa kuongeza wigo wa umri wa wanufaika wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka ukomo wa umri wa miaka 18 mpaka umri wa miaka 21.

Aidha, Rugambwa amesisitiza kuwa TALGWU mkoa wa Singida iko tayari kwa mapokezi ya Mheshimiwa Rais na inawahamasisha wafanyakazi wote kujitokeza kwa wingi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “ Uchaguzi Mkuu wa 2025 utuletee viongozi wanaojali na kuthamini haki na maslahi ya wafanyakazi, Sote tushiriki.”

#MeiMosi2025 #SamiaNaSingida #SamiaThegameChanger

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *