OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

RAIS SAMIA AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba muhimu mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya Ikulu. #RaisSamia #MawaziriWapya #Ikulu #HotubaYaRais #Tanzania

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AMEKABIDHIWA RASMI OFISI NA WAZIRI MKUU MSTAAFU KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alikabidhiwa rasmi ofisi na Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa Novemba 17, 2025, Mlimwa, Dodoma. Hafla ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Doto Biteko, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Soma zaidi »

DKT. MWIGULU AAPISHWA IKULU CHAMWINO—RAIS SAMIA AELEZA SABABU ZA UTEUZI WAKE

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika hotuba yake, Rais Samia amesema uteuzi huo ulipitia ushindani mkubwa na Dkt. Mwigulu ndiye aliyebeba sifa nyingi zaidi kwenye vigezo vyote vilivyopimwa. Ameeleza kuwa majukumu ya Waziri Mkuu …

Soma zaidi »

RAIS DKT. SAMIA AKIMUAPISHA MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla inayofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma, tarehe 14 Novemba, 2025.

Soma zaidi »

BREAKING NEWS: MWIGULU NCHEMBA ATANGAZWA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI 🇹🇿

Leo bungeni, Spika ametangaza rasmi uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangazo hilo limepokelewa kwa shangwe na pongezi kutoka kwa wabunge na wananchi nchini kote. Tazama video hii kwa taarifa kamili kutoka Bungeni Dodoma na maoni ya viongozi mbalimbali. #Tanzania #MwiguluNchemba #WaziriMkuu …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kwa dhati mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo BAKWATA na wadau wote wa elimu katika kuimarisha maadili, kuendeleza maarifa na kuleta mshikamano wa kitaifa kupitia elimu.

Amesema kuwa elimu haiwezi kukamilika kama hakuna maadili kwani ndiyo yanayojenga utu, heshima na mshikamano wa kijamii. “Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu inakuza maarifa na ujuzi, sambamba na malezi yanayoimarisha tabia bora na maadili ya kizalendo kwa vijana wa Kitanzania”. Amesema hayo Jumamosi Septemba …

Soma zaidi »

MAENDELEO YANAKUJA KWA KUFANYA KAZI – DKT. BITEKO

“Tangu kuanza kwa mradi wa EACOP mwaka 2022 hadi sasa, jumla ya Watanzania 9,194 wamepata nafasi za kufanya kazi ndani ya mradi na hivyo kuwa fursa kwao ya kujipatia kipato, mwaka 2024 kampuni ilitoa mafunzo maalumu kwa Vijana 170 na kuwapatia kazi kwenye mradi, Vijana wengine 110 wapo katika masomo …

Soma zaidi »

SHEREHE ZA UFUNGAJI RASMI WA MAONESHO YA 49 SABASABA | WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ameongoza sherehe ya kufunga rasmi Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA), yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba – Barabara ya Kilwa. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa maonesho …

Soma zaidi »