Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kwa dhati mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo BAKWATA na wadau wote wa elimu katika kuimarisha maadili, kuendeleza maarifa na kuleta mshikamano wa kitaifa kupitia elimu.

Amesema kuwa elimu haiwezi kukamilika kama hakuna maadili kwani ndiyo yanayojenga utu, heshima na mshikamano wa kijamii. “Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu inakuza maarifa na ujuzi, sambamba na malezi yanayoimarisha tabia bora na maadili ya kizalendo kwa vijana wa Kitanzania”.

Image

Amesema hayo Jumamosi Septemba 20, 2025 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia katika hafla ya usiku ya utoaji tuzo za elimu za mufti iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serena hotel jijini Dar es Salaam.

“Rais Dkt. Samia anawapongeza sana BAKWATA kwa juhudi kubwa mnazozifanya katika masuala yote ya maendeleo ya jamii hususan mchango wenu katika kuendeleza elimu na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia malezi ya maadili na maarifa, Serikali inathamini sana mchango wa taasisi za dini kama BAKWATA katika kuunga mkono malezi ya watoto na vijana”. Amesema Mheshimiwa Majaliwa.

Image

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limekuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya elimu nchini kwani limeanzisha na kuendesha shule, madrasa na vyuo vinavyotoa elimu bora ya dini na ya kawaida, sambamba na kujenga maadili mema kwa vijana.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *