MatokeoChanya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikagua mabanda ya maonesho ya wadau wa sekta ya maji nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam kabla ya kufungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Kisayansi la Maji linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Jumatano Januari 29, 2025 mpaka Ijumaa Januari 31, 2025

Soma zaidi »

MELEFU WAJITOKEZA KUPATA ELIMU NA MSAADA WA KISHERIA UZINDUZI MSLAC MKOA WA 17 WA KILIMANJARO TAREHE 29/1/2025

Kampeni ya Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) imepiga hatua kubwa tangu ilipoanzishwa, na uzinduzi wa mkoa wa 17 Kilimanjaro mnamo 29 Januari 2025 ni uthibitisho wa mafanikio yake katika kuenea kitaifa. Hapa ni tathmini ya maendeleo ya kampeni hii tangu kuanzishwa kwake: 1. Ufanisi wa Kampeni Hadi Sasa – MSLAC …

Soma zaidi »

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya Mazungumzo na NaibuMkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Bo Li

Mazungumzo hayo yalifanyika kando ya Mkutano waNishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika unaofanyikakatika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)

Soma zaidi »

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu (Asian Infrastructure Investment Bank – AIIB), Bw. Jin Luqun

Wamekutana na kuzungumza kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza (27.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano wa katika kuboresha miundombinu nchini, ukiwemo Mradi wa …

Soma zaidi »

Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye, alipowasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati

Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye yuko nchini kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaowakutanisha Viongozi wa Nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la …

Soma zaidi »

Rais wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati

Mkutano huo unafanyika nchini kuanzia leo Januari 27 hadi kesho Januari 28, 2025, katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Kiongozi huyo alilakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk Saada Mkuya, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano …

Soma zaidi »

Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama amewasili jijini Dar es Salaam Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere

Mhe. Mahama amepokelewa na Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso. Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Lengo ni kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na …

Soma zaidi »

RAIS WA ZAMBIA AWASILI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA MKUTANO WA NISHATI

Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema, amewasili jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika nchini kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, …

Soma zaidi »