Tanzania imefanikiwa kufanikisha ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii wa ndani kati ya mwaka 2021 na 2024, ikivunja rekodi za awali. Mafanikio haya yanatokana na juhudi thabiti na uongozi makini wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni mbalimbali za kimkakati.
Moja ya juhudi kubwa za Mheshimiwa Rais ni uzinduzi wa filamu maarufu ya Royal Tour mwaka 2022, ambayo ilionyesha uzuri wa vivutio vya asili na kiutamaduni vya Tanzania kwa ulimwengu. Filamu hiyo ilifanikiwa si tu kuvutia watalii wa kimataifa, bali pia kuhamasisha Watanzania wengi kutembelea vivutio vyao vya ndani.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+