USIPOTEZE HAKI YAKO, WAHI KAHAKIKI TAARIFA ZAKO, RAIS DKT. SAMIA

“Ndugu zangu nami nimeona nijiunge nanyi hapa kituoni kwetu. Kama mnavyojua mimi ni mkazi wa Chamwino na nimepiga kura nyingi huko nyuma. Lakini kwa mwaka huu ni lazima nipige hapa Chamwino. Kwa hiyo ndiyo maana nimekuja kurekebisha taarifa zangu.

Si mpiga kura mpya lakini nimekuja kurekebisha taarifa zangu. Huko nyuma nilikuwa napiga Zanzibar kwa sababu nilikuwa Makamu wa Rais, nilikuwa naenda kupiga kule na Rais wa Jamhuri napiga hapa Dodoma.

Lakini Mwaka huu inabii nipige hapa makao makuu ya nchi, ambapo ndiyo makao ya serikali yalipo,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *