SIRI YA MTO USIOISHA, DAWA YA ASILI KUTOKA BARAFU ZA MLIMA KILIMANJARO! KILASIYA WATERFALLS:

Kilasiya ni maporomoko ya maji ya kipekee yaliyopewa jina la Kichaga lenye maana ya “kitu kisichoisha.” Maporomoko haya hayakauki hata wakati wa kiangazi, tofauti na maporomoko mengine manne ya Marangu. Kilasiya ilianzishwa mwaka 1991 na Libori George Mosha, Mkazi wa Marangu, kijiji cha Kyala, mkoani Kilimanjaro, kama mradi wa kutunza mazingira.

Chanzo cha maji yake ni barafu inayoyeyuka kutoka Mlima Kilimanjaro, na maji haya husafiri hadi bwawa la Nyumba ya Mungu kwa ajili ya kuzalisha umeme. Kilasiya Waterfalls inajulikana kwa maji masafi yanayoweza kunyweka moja kwa moja bila kuchemshwa, na yanadaiwa kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa kama gauti na vipele.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *