
Katika hatua ya kipekee ya kuonyesha uzuri wa mazingira ya Afrika, filamu ya kimataifa Mufasa: The Lion King imeleta mabadiliko makubwa katika jinsi hadithi ya kifalme ya simba inavyoonyeshwa. Mchanganyiko huu wa mandhari halisi na hadithi ya kusisimua unaleta uzuri wa Afrika, ukionyesha maeneo ya kipekee kutoka kwenye majangwa ya Namibia hadi maporomoko ya Victoria. Hata hivyo, sehemu ya pekee ya hadithi hii inatokana na mandhari ya Tanzania, ambayo imetoa mchango mkubwa kwa filamu hii ya Walt Disney Pictures. imepigwa na Mpigapicha wa mitandao ya “#matokeochanya na #sisinitanzania Mussa Ally Mbwego (#kakamussa)

TUNAKUPONGEZA KWA DHATI KAKA MUSSA.
Ubunifu wa Teknolojia ya Drone katika Mandhari ya Tanzania Katika filamu hii, teknolojia ya uhuishaji wa dijitali imetumiwa kwa umakini mkubwa ili kuwasilisha uzuri asilia wa maeneo ya Tanzania. Kaka Mussa umeonyesha umahili mkubwa kuendesha drone, Umeweza kurekodi mandhari ya kipekee kutoka maeneo kama: Iringa – Isimila Pillars: Picha hizi zinadhihirisha sura za ajabu na historia ya geolojia ya Tanzania.
Ziwa Natron: Mwangaza wa asili na mandhari ya kuvutia ya ziwa hili limeleta mvuto wa kipekee katika hadithi.
Ngorongoro Crater: Moja ya maajabu ya kiasili ya Tanzania, ambayo imekuwa chanzo cha mvuto wa wasanii na watayarishaji wa filamu duniani.
Zaidi ya hayo, picha zilizopatikana zimeweka katika muktadha wa historia ya Olduvai na uzuri wa nyasi za Serengeti na Maasai Mara, zikionyesha mchanganyiko wa tamaduni na mandhari ambayo ni sehemu ya utajiri wa Afrika. Pongezi Kaka Mussa. NINI KIFANYIKE TANZANIA INUFAIKE ZAIDI?
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+