MKAZI WA ARUSHA AACHANA NA DAWA ZA KULEVYA, AANZISHA SHAMBA LA MAZAO YA CHAKULA

Talik Azizi Mkawa, mkazi wa Arusha, ni mfano wa kuigwa baada ya kuamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kuanza ukurasa mpya wa maisha.

Baada ya kupata nafuu, Talik amesema aliguswa na wito wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyewahimiza vijana waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya kujikita katika kazi halali ili kujikimu kimaisha na kujenga taifa lenye nguvu ya uzalishaji. Akiwa na baadhi ya wenzake, Talik waliamua kuanzisha shamba linalozalisha mazao mbalimbali ya chakula ikiwemo maharage, mihogo, migomba, mboga mboga na mpunga.

Anaeleza kuwa hatua hiyo imekuwa chanzo cha matumaini mapya si tu kwao binafsi, bali pia kwa vijana wengine waliokuwa wamekata tamaa kutokana na athari za uraibu. Kwa Talik, kazi imekuwa tiba, heshima na njia ya kurejesha utu wake. Anasisitiza kuwa kila kijana anaweza kubadilika na kujijenga upya ikiwa atachukua hatua na kuamua kuishi maisha yenye malengo.

#KataaDawaZaKulevyaTimizaMalengoYako #DCEA #piga119

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba muhimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *