SERIKALI YA RAIS SAMIA YAWEKA MSINGI IMARA WA KUMPA KILA MTANZANIA HESHIMA NA FURSA

Utu wa mtu ni nguzo muhimu kwa kila binadamu, bila kujali anapitia hali gani katika maisha. Thamani ya utu haiwezi kupimwa kwa mali, cheo, au nafasi bali kwa jinsi tunavyomtendea binadamu mwenzetu.

Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeonyesha kwa vitendo kwamba utu ni kipaumbele katika maendeleo ya taifa. Ujenzi wa kituo cha matibabu ya waraibu wa dawa za kulevya cha Methadone huko Kihonda ni mfano halisi wa serikali inayojali utu.

Hii ni hatua ya kipekee inayolenga kuwasaidia wale waliokuwa wakipitia changamoto za uraibu, wakiwemo wanaotumikia vifungo, kurejea katika jamii wakiwa na afya njema na matumaini mapya. Vilevile, jitihada za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulenya (DCEA) kurejesha mazao mbadala kwa wakulima waliokuwa wakilima mazao haramu kama bangi na mirungi zinaonyesha dhamira ya kweli ya kujenga jamii yenye fursa halali za kipato.

Badala ya adhabu pekee, serikali imechagua njia ya kutoa suluhisho kuwainua wananchi kiuchumi huku ikilinda utu wao. Kwa maneno mengine, sera na hatua hizi zinaweka wazi kwamba maendeleo ya kweli ni yale yanayomgusa mwanadamu moja kwa moja kwa kumheshimu, kumsaidia, na kumpa nafasi ya pili. Utu ni msingi wa maendeleo endelevu, na serikali ya Rais Samia imeweka alama ya wazi kwamba Tanzania ya sasa ni nchi inayomjali mtu kabla ya mfumo.

#KataaDawaZaKulevyaTimizaMalengoYako #DCEA

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba muhimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *