Sekta ya utalii nchini Tanzania imefikia na hata kuvuka malengo yaliyowekwa kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024, hatua inayodhihirisha mafanikio makubwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia juhudi za kimkakati, ikiwemo uzinduzi wa filamu ya Royal Tour, uwekezaji katika miundombinu ya kitalii, na kampeni za uhamasishaji wa utalii wa ndani na kimataifa, Tanzania imefanikiwa kufanikisha ukuaji wa sekta hii kwa viwango vya kihistoria.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii, utalii wa ndani umeongezeka kwa asilimia 307.9%, huku utalii wa kimataifa ukikua kwa asilimia 132.1% ndani ya miaka minne. Ukuaji huu umepita matarajio, na sekta ya utalii imekuwa moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya taifa, ikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mafanikio haya yameongeza nafasi za ajira, kuimarisha biashara zinazohusiana na utalii, na kuhamasisha Watanzania kufurahia utajiri wa asili na utamaduni wa nchi yao. Tanzania sasa inajivunia nafasi yake kama kiongozi wa utalii barani Afrika na mfano wa jinsi juhudi thabiti za serikali zinavyoweza kuleta mabadiliko makubwa.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+