Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ameongoza sherehe ya kufunga rasmi Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA), yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba – Barabara ya Kilwa. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa maonesho …
Soma zaidi »Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025. Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri ni cha mwisho cha Serikali ya Awamu ya Sita kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuendeleza juhudi za kutafuta masoko ya nje ili kuongeza mauzo yatakayowezesha nchi kupata fedha za Kigeni.
Amesema kuwa TanTrade inapaswa kufanya tafiti za uhakika na uchambuzi wa masoko ambayo bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa na kutoa taarifa hizo kwa wafanyabiashara kote nchini. Ametoa agizo hilo (Jumapili, Julai 13, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya …
Soma zaidi »MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MTEULE DKT. DANIEL MONO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Julai 13, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kumweka wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Dkt. Daniel Henry Mono wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mwanga. Ibada hiyo imefanyika katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Soma zaidi »WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi
Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla na ni moja ya sababu inyowezesha maendeleo ya Taifa kwenda kwa kasi. Amesema hayo leo Alhamisi (Julai 03, 2025) wakati wa uzinduzi wa Benki ya Maendeleo PLC, kuwa Benki kamili ya kibiashara, …
Soma zaidi »Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa nguzo ya kuimarisha mshikamano na umoja wa kitaifa na kufanikisha maendeleo katika sekta mbalimbali za maendeleo
Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wake, Rais Dkt. Samia ameweza kusimama imara katika kuendeleza miradi ya kimkakati na huduma za jamii, kusimamia demokrasia, kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia. Amesema hayo leo (Alhamisi, Juni 26, 2025) wakati alipotoa hoja ya kukamilisha shughuli za Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma. “sina …
Soma zaidi »RAIS DKT. SAMIA ANATAMBUA MCHANGO WA BUNGE KWENYE KUHAMAISHA MICHEZO-MAJALIWA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika tamasha la Grand Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma.
Soma zaidi »WAZIRI MKUU MGENI RASMI KILELE MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TET
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Juni 17, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yanayofanyika katika Bamaga Jijini Dar es Salaam.
Soma zaidi »LIVE:WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA – DAR ES SALAAM
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, amezindua rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia jijini Dar es Salaam. Kampeni hii inalenga kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wote, hususan makundi yenye uhitaji kama wanawake, vijana, wazee, na watu wenye …
Soma zaidi »