Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza matembelezi ya hisani na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TET) ambapo amesisitiza uongozi wa taasisi hiyo kuongeza wigo wa kuimarisha upatikanaji wa vitabu kwenye shule zote nchini
Waziri Mkuu amesema anafahamu kuwa TET imedhamiria kuchapa vitabu kwa wingi ili kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja, jambo ambalo litaleta manufaa makubwa katika elimu na Taifa kwa ujumla. “Hivyo, kwa dhamira ya dhati kabisa, sote hatuna budi kuliunga mkono jambo hili.” Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi …
Soma zaidi »WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika kesho Januari 15, 2025. Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO …
Soma zaidi »Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Januari 14, 2025 amefanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe aliofuatana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha mabondia kunufaika na vipaji vyao.
Ametoa Wito huo jana (Alhamisi, Desemba 26, 2024) wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam. “Awali michezo hii ilikuwa ni ridhaa, lakini kwasasa tumeweka sheria ambazo zinataka mchezo huu uwe wa kulipwa, ambayo mchezaji …
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipopiga simu kuzungumza na wadau na Mashabiki wa mchezo wa ngumi, wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 pamoja na barabara unganishi yenye urefu wa kilomita 2.3
Hafla hiyo ilifanyika katika mkoa wa Simiyu, ambapo Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ipo imara na imejidhatiti kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wote nchini. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Majaliwa aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi …
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 20, 2024 amezindua nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba mwaka jana katika kijiji cha Gendabi wilayani Hanang Mkoa wa Manyara
Pichani, Waziri Mkuu akizungumza na Brightina Francis wa kijiji cha Gendabi baada ya kuzindua nyumba hizo zilizojengwa katika kitongoji cha Waret wilayani humo
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kuaga mwili wa marehemu John Billy Tendwa ambaye aliwahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Akitoa Salama pole kwa waombolezaji wakati wa tukio la kuaga lililofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji kuyaenzi mema yote aliyoyafanya marehemu Tendwa katika kipindi cha uhai wake. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Marehemu Tendwa …
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vyote vya usalama vihakikishe watu wote waliokwama ndani ya jengo lililoporomoka katika kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wanaokolewa huku mali zao zikilindwa.
Ametoa agizo hilo (Jumamosi, Novemba 16, 2024) baada ya kushuhudia juhudi za uokoaji zinavyoendelea baada ya jengo ghorofa nne kuporomoka katika eneo la Karikoo. Akizungumza baada ya kukagua juhudi za uokoaji katika eneo hilo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Majaliwa amesema hadi sasa watu 40 mejeruhiwa ambapo …
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+