Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZIKO YA MAREHEMU LAWRENCE MAFURU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 15, 2024 ameungana na ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wengine wa Serikali katika mazishi ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru. Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Kondo, Ununio jijini Dar es Salaam. Marehemu Mafuru alifariki Novemba 09, 2024 …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Marehemu Lawrence Mafuru kwenye viwanja vya Karimjee

Tukio la kuaga mwili wa Marehemu Lawrence Mafuru liliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Soma zaidi »

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi

Amesema kuwa maboresho hayo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki yatasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya karatasi katika vikao vya Serikali, hususan Baraza la Mawaziri, hivyo kupunguza changamoto ikiwemo kuchelewa kwa taarifa, gharama kubwa za uchapaji na hatari ya upotevu wa taarifa muhimu. Amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 11, …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAISLAMU WA SHIA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 10, 2024 amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kongamano hilo linaloratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa SHIA Tanzania, lilofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji wote Serikalini wahakikishe vipaumbele vilivyoanishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026 vinatafsiriwa vema kwenye mipango ya Taasisi zao

Amesema mpango huo umejikita katika kuendeleza na kukamilisha utekelezaji wa afua zinazotoa matokeo ya maeneo matano ya kipaumbele ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 8, 2024) wakati akiahirisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 12 Bungeni jijini Dodoma, …

Soma zaidi »

ZINGATIENI MISINGI YA UTAWALA BORA KATIKA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wasimamizi wote wa rasilimaliwatu wazingatie misingi ya utawala bora na weledi katika kuisimamia rasilimali hiyo katika Sekta ya Umma Barani Afrika. Amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha kutoa huduma bora na kudumisha imani ya wananchi kwa Serikali zao. Ametoa wito …

Soma zaidi »

Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali una mchango gani katika uimarishaji wa utawala bora?

Serikali imezindua rasmi mifumo ya kidijitali kwenye taasisi za umma ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, kuongeza ufanisi, na kupunguza urasimu. Hatua hii inachukuliwa kama sehemu ya jitihada za serikali za kuendana na maendeleo ya kiteknolojia na kuweka mazingira bora ya utawala wa kisasa. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliongoza …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU: SERIKALI IMEIMARISHA NGUVUKAZI SEKTA YA AFYA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeimarisha nguvukazi kwenye sekta ya afya kwa kuongeza taasisi zinazotoa mafunzo ya afya na upatikanaji wa fursa za elimu ya juu kwa kada hiyo. “Serikali imefanya upanuzi wa taasisi za mafunzo ya afya ili kuongeza idadi ya wahitimu. Taasisi hizo ni pamoja na vyuo …

Soma zaidi »