MatokeoChanya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhwan Jakaya Kikwete (Mb), ametoa hotuba muhimu, Agosti 27, 2025, Dar es Salaamu JengO la Nsssf ,Wakati wa ziara ya Mheshimiwa Gembá Koichiro, Makamu Spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan, na ujumbe wake

Hotuba hiyo ililenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu, hasa vijana. Mhe. Kikwete alieleza kuwa Tanzania imeendelea kuwa na ukuaji thabiti wa uchumi, lakini ili kufungua kikamilifu uwezo wake, ni lazima kuwa na kipaumbele katika maendeleo …

Soma zaidi »

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemteua Mhe. Mhe. Majalio Paul Kyara kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Satia Mussa Bebwa kugombea Kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU)

Hafla hiyo ya uteuzi iliyofanyika kwenye Ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma tarehe 27 Agosti, 2025 imeongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele. #KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura #uchaguzi2025 #uchaguzi #tumehuruyataifayauchaguzi #uchaguzimkuu

Soma zaidi »

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu Kailima R.K, amefunga kikao cha siku mbili cha Tume na Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili kamili na ambavyo vimependekeza wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais. Kikao hicho kiliitishwa kwa lengo la kujadili na kupanga kwa pamoja ratiba ya kampeni za vyama hivyo

Kikao hicho kilichoketi Agosti 25 na 26, 2025 kilishirikisha vyama vya Civic United Front (CUF), National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha Mapinduzi (CCM), National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party …

Soma zaidi »

DKT. SAMIA AANZA RASMI SAFARI YA UCHAGUZI – ACHUKUA FOMU NEC KWA USHINDI WA CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, amechukua rasmi fomu ya uteuzi katika Tume Huru ya Uchaguzi, kuashiria mwanzo wa safari ya uchaguzi kwa chama tawala. Tukio hili limehudhuriwa na viongozi waandamizi wa CCM, wafuasi, na wananchi …

Soma zaidi »