Baadhi ya Wafanyakazi nchini wametoa pongezi na shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuthibitisha tena kuwa anawajali watumishi wa umma. Katika kilele cha sherehe za Mei Mosi 2025 zilizofanyika Uwanja wa Bombadia mkoani Singida, Rais Samia alitangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 35.1, kutoka Shilingi 370,000 hadi Shilingi 500,000.
Wafanyakazi wamesema hatua hiyo ni ishara ya uongozi wenye huruma, usikivu na uthubutu wa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watumishi. Aidha, ahadi ya kuongeza mishahara kwa ngazi nyingine kulingana na uwezo wa bajeti imeongeza matumaini mapya ya ustawi wa kazi.
Wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, wakilipa mema kwa mema.
#MeiMosi2025 #KazinaUtuTunasongaMbele #WafanyakaziTanzania
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+