Mwenyekiti wa Chama cha ADA TADEA Mkoa wa Songea, Alli Sadiki Mapunda, ametangaza kuwa chama chao kipo tayari kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa ADA TADEA itasimamisha wagombea katika nafasi zote za udiwani na ubunge, lakini kwa nafasi ya urais, chama hicho hakitasimamisha mgombea wake bali kitaunga mkono Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais aliyepo madarakani, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mapunda amefafanua kuwa uamuzi huo umetokana na kuthamini juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi yanaenda sambamba na maboresho ya mazingira ya kisiasa, ikiwemo kusikiliza malalamiko ya vyama vya upinzani.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+