TUME YA UCHAGUZI

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.

Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar. Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025. #KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura #oktoba2025 #tumehuruyataifayauchaguzi #uchaguzi2025 #UchaguziMkuu #uchaguzi

Soma zaidi »

🔴CCM INAZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU 2025 KAWE DAR ES SALAAM, AGOSTI 28, 2025

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mgombea Urais wa Tanzania kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi kampeni za CCM kupitia tiketi ya chama hicho leo tarehe 28 Agosti 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe – Dar es Salaam. Katika uzinduzi huu, …

Soma zaidi »

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemteua Mhe. Mhe. Majalio Paul Kyara kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Satia Mussa Bebwa kugombea Kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU)

Hafla hiyo ya uteuzi iliyofanyika kwenye Ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma tarehe 27 Agosti, 2025 imeongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele. #KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura #uchaguzi2025 #uchaguzi #tumehuruyataifayauchaguzi #uchaguzimkuu

Soma zaidi »

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu Kailima R.K, amefunga kikao cha siku mbili cha Tume na Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili kamili na ambavyo vimependekeza wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais. Kikao hicho kiliitishwa kwa lengo la kujadili na kupanga kwa pamoja ratiba ya kampeni za vyama hivyo

Kikao hicho kilichoketi Agosti 25 na 26, 2025 kilishirikisha vyama vya Civic United Front (CUF), National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha Mapinduzi (CCM), National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party …

Soma zaidi »

DKT. SAMIA AANZA RASMI SAFARI YA UCHAGUZI – ACHUKUA FOMU NEC KWA USHINDI WA CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, amechukua rasmi fomu ya uteuzi katika Tume Huru ya Uchaguzi, kuashiria mwanzo wa safari ya uchaguzi kwa chama tawala. Tukio hili limehudhuriwa na viongozi waandamizi wa CCM, wafuasi, na wananchi …

Soma zaidi »

TUMETENGENEZA UTAMADUNI WA DEMOKRASIA YA UCHAGUZI NI KUTUNZA AMANI KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI.

“Tumetengeneza utamaduni wa demokrasia ya uchaguzi, na sehemu ya utamaduni huo ni kutunza amani kabla na baada ya uchaguzi.” – Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ujumbe huu unasisitiza thamani ya demokrasia tuliyoijenga kama taifa. Uchaguzi siyo tu kura, bali pia ni utamaduni wa kuheshimiana, mshikamano na kulinda amani ya nchi …

Soma zaidi »