RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetunukiwa Tuzo Kuu ya Ubunifu katika Huduma Jumuishi za Fedha (Nestor Espenilla Jr. Financial Inclusion Innovation Award) inayotolewa na Jumuiya ya Huduma Jumuishi za Fedha (AFI), yenye wanachama 84 duniani.

Tuzo hiyo ilipokelewa na Naibu Gavana wa BoT anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, kwa niaba ya Gavana Bw. Emmanuel Tutuba, katika Mkutano Mkuu wa AFI uliofanyika hivi karibuni mjini Swakopmund, Namibia. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 15, 2025 wakati akitangaza tuzo hiyo, …

Soma zaidi »

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Japan Mhe. Anderson Mutatembwa, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amemsihi Balozi Mutatembwa kuzingatia kipaumbele cha nchi ambacho ni diplomasia ya uchumi kwa kuhakikisha anavutia wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchini Japan pamoja na kuimarisha ushirikiano wa ubia. Amemsisitiza Balozi Mutatembwa kuhakikisha makampuni ya Japan yanawekeza nchini Tanzania ili kuongeza thamani ya bidhaa hapa nchini …

Soma zaidi »

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu Kailima, R. K (kulia) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Ndugu Adam Mkina wakishuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – WAZALENDO), Mhe. Luhaga Joelson Mpina na Mgombea Mwenza, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej majira ya Saa 10:00 jioni ya leo (13/9/2025)

Ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria inayotaka fomu hizo kubandikwa kwa Saa 24 ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa …

Soma zaidi »