Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika kutumika kuwekeza katika kuendeleza miundombinu ni vema kuhakikisha michango ya wanachama ambayo imetengwa kama kinga dhidi ya misukosuko ya kiuchumi na kijamii pamoja na kukabiliana na umaskini inabaki kuwa ya kutosha kukidhi malengo ya msingi ya uanzishwaji wake
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Amesisitiza kuwepo umakini kwenye uwekezaji wa miradi ya miundombinu kwani miradi ambayo haiwezi kutekelezeka inaweza kudhoofisha …
Soma zaidi »Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amepongeza uwepo wa kituo cha Umahiri cha Matibabu cha Afrika (AMCE) ambacho amesema kitakua mfano kwa bara la Afrika na kusaidia kuokoa gharama kupeleka wagonjwa nje ya bara hilo
Makamu wa Rais amesema hayo alipotembelea Kituo cha Umahiri cha Matibabu ya Kibingwa cha Afrika kilichopo Abuja nchini Nigeria. Amesema kituo hicho kitasaidia kuhamisha maarifa na hivyo kuwezesha wazawa kuweza kutoa huduma za afya endelevu kwa wananchi wa Afrika. Amewapongeza wataalamu ambao walihudumu katika hospitali mbalimbali nje ya Afrika kwa …
Soma zaidi »Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Afrexim Prof. Benedict Okey Oramah. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa 32 wa Benki ya Afrexim unaofanyika Abuja nchini Nigeria leo tarehe 26 Juni 2025
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Jijini Abuja nchini Nigeria leo tarehe 25 Juni 2025
Makamu wa Rais anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 32 wa Benki ya Afrexim utaokaofanyika tarehe 25-27 Juni 2025.
Soma zaidi »