Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Amesisitiza kuwepo umakini kwenye uwekezaji wa miradi ya miundombinu kwani miradi ambayo haiwezi kutekelezeka inaweza kudhoofisha uwezo wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutimiza wajibu wake.

Aidha Makamu wa Rais amesema ni muhimu tahadhari ichukuliwe ili kuepusha miradi iliyobuniwa vibaya, yenye gharama kubwa kupita kiasi au miradi migumu kupita kiasi ambayo ni ngumu kuisimamia na ile isiyokidhi mahitaji ya walengwa wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Ameongeza kwamba iwapo upembuzi yakinifu na thabiti wa miradi ya miundombinu hautafanywa mapema inaweza kusababisha kuchelewa kwa malipo ya walengwa au hata kushindwa kabisa kuirejesha.

Vilevile Makamu wa Rais amewahimiza wataalamu wanaohudhuria mkutano huo kuandaa mikakati ya jinsi gani Mifuko bora ya Hifadhi ya Jamii inaweza kuchangia katika kuongeza juhudi zinazoendelea za kuongeza ufadhili wa uwekezaji katika miundombinu ya kijamii na kiuchumi maeneo ya vijijini. Amesema uwekezaji katika miundombinu ya vijijini utasaidia kuongeza tija na ubora wa maisha katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji, kutengeneza ajira na kupunguza uhamaji wa wananchi kutoka vijijini kwenda mijini.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+