Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 15, 2024 ameungana na ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wengine wa Serikali katika mazishi ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru. Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Kondo, Ununio jijini Dar es Salaam. Marehemu Mafuru alifariki Novemba 09, 2024 …
Soma zaidi »MatokeoChanya
Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza ushirikishaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa nchini Tanzania. Ameweka msisitizo kwenye kuboresha usalama wa chakula kupitia mipango mbalimbali inayolenga kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wananchi wote
Katika mkutano wa G20 unaotarajiwa kufanyika Rio de Janeiro, Brazil, tarehe 18 hadi 19 Novemba 2024, Rais Samia amealikwa kushiriki kama mgeni mwalikwa. Ushiriki wake katika mkutano huu ni fursa muhimu kwa Tanzania kuwasilisha ajenda zake kuhusu usalama wa chakula na ushirikishaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa. Kupitia …
Soma zaidi »“KUJENGA ULIMWENGU WA HAKI NA SAYARI ENDELEVU”
#SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya #kilimochakisasa
Soma zaidi »Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa wafiwa wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru katika Viwanja vya Karimjee
Mhe. Dkt. Kikwete alifika hapo akitokea Uwanja wa Ndege moja kwa moja akitokea kuhudhuria vikao vya Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Elimu Duniani (GPE), ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, jijini Washington DC, Marekani.
Soma zaidi »Tanzania Itakuwa Bora Na Imara Ikiwa Kila Mmoja Wetu Atatimiza Wajibu Wake Wa Msingi
Wapendwa Watanzania wenzangu, wakati wa kuchagua viongozi wetu unakaribia. Ni fursa adhimu na ya kipekee kwa kila mmoja wetu kuamua mustakabali wa taifa letu. Kupiga kura ni haki yetu ya msingi, lakini zaidi ya haki ni wajibu wa kila mmoja katika kujenga Tanzania tunayoitaka.
Soma zaidi »Huu Ndio Wakati Wetu Wa Kuonesha Uzalendo Kwa Vitendo Kwa Taifa Letu, Tujitokeze Tukapige Kura!
Tanzania mbele kwa kura yako! Huu ndio wakati wetu wa kuonesha uzalendo kwa vitendo na kuimarisha taifa letu. Kwa pamoja, tukitoa sauti zetu kwa njia ya kura, tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Hivyo basi, tusikose kutimiza wajibu huu muhimu wa kitaifa.
Soma zaidi »“Tujitokeze Tupige Kura Kwa Viongozi Wanaotamani Kuona Tanzania Ikisonga Mbele”
Tusikubali kusimama pembeni wakati wa uamuzi muhimu. Kwa pamoja, tukiwa na umoja na uzalendo, tujitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura, tuweke sauti yetu kwa viongozi wanaotamani kuona Tanzania ikisonga mbele. Tukumbuke kuwa kila kura ina umuhimu na maana kubwa kwa mustakabali wa nchi yetu.
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Marehemu Lawrence Mafuru kwenye viwanja vya Karimjee
Tukio la kuaga mwili wa Marehemu Lawrence Mafuru liliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Soma zaidi »Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi
Amesema kuwa maboresho hayo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki yatasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya karatasi katika vikao vya Serikali, hususan Baraza la Mawaziri, hivyo kupunguza changamoto ikiwemo kuchelewa kwa taarifa, gharama kubwa za uchapaji na hatari ya upotevu wa taarifa muhimu. Amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 11, …
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+