DCEA INAJUKUMU LA KUDHIBITI DAWA ZOTE ZA KULEVYA TANZANIA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ni chombo cha serikali chenye jukumu la kusimamia, kudhibiti na kupambana na matumizi, biashara na usambazaji wa dawa zote za kulevya ambazo ni haramu nchini.

DCEA hufanya kazi ya kuzuia uingizaji na utengenezaji wa dawa hizi, kuteketeza mashamba ya mimea haramu kama bangi na mirungi, pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara yake kiafya, kiuchumi na kijamii.

Pia hufanya upelelezi, kushirikiana na vyombo vya kimataifa na kusimamia utekelezaji wa sheria ili kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na huru dhidi ya dawa za kulevya.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inashiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika jijini Dodoma. Usikose! Kataa dawa za kulevya, timiza malengo yako.

Unaweza kuangalia pia

🔴 LIVE: SAMIA SULUHU HASSAN AINGIA KWA KISHINDO MBEYA – MBALIZI

Rais Samia Suluhu Hassan amewasili Mbalizi, Mbeya, kwa kishindo kikubwa akipokelewa na umati wa wananchi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *