Maktaba ya Kila Siku: July 14, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025. Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri ni cha mwisho cha Serikali ya Awamu ya Sita kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.

Soma zaidi »

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuendeleza juhudi za kutafuta masoko ya nje ili kuongeza mauzo yatakayowezesha nchi kupata fedha za Kigeni.

Amesema kuwa TanTrade inapaswa kufanya tafiti za uhakika na uchambuzi wa masoko ambayo bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa na kutoa taarifa hizo kwa wafanyabiashara kote nchini. Ametoa agizo hilo (Jumapili, Julai 13, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya …

Soma zaidi »

UTAMADUNI NDIO UNABAKI KUWA UTAMBULISHO WETU – MHE RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Kauli ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inasisitiza thamani ya urithi wetu wa kiutamaduni kama uti wa mgongo wa taifa. Katika hotuba hii ya kihistoria, Rais anaangazia namna mila, desturi na sanaa zetu zinavyobeba hadhi, heshima na historia ya Watanzania. Tazama video hii kujionea msisitizo wa Serikali ya Awamu …

Soma zaidi »