Katika hotuba yake ya kugusa moyo kwenye Maonyesho ya Sabasaba 2025, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Cyprian Luhemeja, ametahadharisha kuwa dunia imeingia kwenye sura mpya ya mapambano – si tena kwa kutumia silaha, bali dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema janga hili linagusa kila sekta: kilimo kinadorora, vyanzo vya maji vinakauka, na maisha ya mamilioni yako hatarini. Akiwa mstari wa mbele katika kuhimiza hatua za haraka, Eng. Luhemeja anatoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira kwa vitendo na kuunga mkono jitihada za serikali na wadau mbalimbali.
Tazama video hii usikilize ujumbe wake mzito na ujifunze ni kwa namna gani kila mmoja anaweza kuwa sehemu ya suluhisho.
#MabadilikoYaTabianchi #EngLuhemeja #Sabasaba2025 #VitaMpya #OfisiYaMakamuWaRais #MazigiraKwanza #DITF2025
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+