ALIYEKUWA MRAIBU WA DAWA ZA KULEVYA ATOA SHUKRANI KWA DCEA KWA KUMREJESHA KUISHI MAISHA MAPYA

Rehema Peter Mjindo, mmoja wa waathirika wa zamani wa dawa za kulevya, ameeleza kwa furaha jinsi alivyofanikiwa kuachana kabisa na matumizi ya dawa za kulevya kupitia msaada alioupata kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA). Rehema amesema kuwa kupitia huduma ya matibabu na ushauri aliopewa, alifanikiwa kupata nafuu na sasa anajitegemea kwa kufanya shughuli za ujasiriamali alizofundishwa kupitia mafunzo ya SIDO.

“Naishukuru kwa elimu ya ujasiriamali na matibabu niliyopatiwa. Leo hii naishi maisha huru, na ninawaelimisha wengine jinsi ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya,” amesema Rehema kwa uchangamfu.

Rehema pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha DCEA kifedha na kiteknolojia, hali ambayo imesaidia kuwafikia waathirika wengi zaidi nchini. Ametoa wito kwa vijana wengine walio katika lindi la dawa za kulevya kujitokeza ili kupata msaada.

Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”

#DCEA #OktobaTunatiki #Sabasaba2025

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *