Recent Posts

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuzingatia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili kulinda ustawi wa wafanyakazi na kuongeza tija ya uzalishaji.

Waziri Sangu ametoa wito huo (Januari 05, 2026) mkoani Mwanza, wakati wa ziara yake maalum ya kukagua utekelezaji wa masuala ya  Usalama na Afya Mahali Pa Kazi katika Kiwanda cha Omega Fish Limited. Akiwa kiwandani hapo Waziri Sangu amepongeza menejimenti ya kiwanda hicho kwa kutoa ajira kwa wazawa na kuzingatia …

Soma zaidi »