Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Mhe. Stephen Wasira

Mazungumzo hayo yalifanyika wakati wakisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Dodoma kwa usafiri wa Treni ya Umeme ya Kisasa (SGR) leo tarehe 08 Machi 2025

Soma zaidi »

“MKOA WA ARUSHA NI MKOA MAMA WA MIKUTANO YA KIMATAIFA” MAKONDA.

Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuhakikisha Arusha inazidi kung’ara kama kitovu cha mikutano ya kimataifa. Uwekezaji mkubwa katika miundombinu na mazingira bora ya mikutano umeifanya Arusha kuwa chaguo kuu kwa matukio makubwa ya kimataifa, kukuza utalii, biashara, na diplomasia. 🔹 Tazama picha chache kutoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani …

Soma zaidi »

TANZANIA YAJITOSHELEZA KWA CHAKULA KWA ASILIMIA 128, RAIS SAMIA ATHIBITISHA MAFANIKIO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa nchi imefanikiwa kuondoa njaa kwa asilimia 100, huku ikijitosheleza kwa chakula kwa asilimia 128. Akizungumza kuhusu hali ya usalama wa chakula nchini, Rais Samia alibainisha kuwa mafanikio haya yanatokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali katika sekta …

Soma zaidi »

📍 BILIONI 300 ZAJENGA UWANJA WA MICHEZO ARUSHA – MAKONDA AMSHUKURU RAIS SAMIA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makonda, amepongeza juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa bilioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa michezo mkoani Arusha. Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Makonda alieleza kuwa uwanja huu utakuwa chachu ya maendeleo ya michezo, kuinua vipaji …

Soma zaidi »

MAKONDA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA, ATOA WITO KWA TLS KUJITOKEZA ZAIDI!

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makonda, amepongeza juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha na kuendeleza kampeni ya msaada wa kisheria kwa wananchi, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, hususan kwa makundi yenye uhitaji mkubwa. Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda ameiomba Chama …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza matembelezi ya hisani na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TET) ambapo amesisitiza uongozi wa taasisi hiyo kuongeza wigo wa kuimarisha upatikanaji wa vitabu kwenye shule zote nchini

Waziri Mkuu amesema anafahamu kuwa TET imedhamiria kuchapa vitabu kwa wingi ili kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja, jambo ambalo litaleta  manufaa makubwa katika elimu na Taifa kwa ujumla. “Hivyo, kwa dhamira ya dhati kabisa, sote hatuna budi kuliunga mkono jambo hili.”   Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi …

Soma zaidi »

🔴#Live: RAIS SAMIA ANASHIRIKI KWENYE MJADALA WA WAKUU WA NCHI AFRIKA MASHARIKI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameongoza Mkutano wa 24 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika jijini Arusha. Mkutano huu umewaleta pamoja viongozi wa nchi wanachama kujadili masuala muhimu yanayoathiri kanda na mustakabali wa jumuiya. Mantiki ya Mjadala: Ufadhili Endelevu wa Jumuiya: Wakuu …

Soma zaidi »

RAIS DKT. SAMIA AZINDUA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI, WANANCHI WAPONGEZA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, iliyopo Mkata-Mbweni, mkoani Tanga. Hospitali hii inajumuisha majengo 15, ikiwa ni pamoja na wodi za wanawake, wanaume, na watoto, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, jengo la upasuaji, huduma za dharura …

Soma zaidi »