RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Shule ya Sekondari ya Geita Girls imekuwa miongoni mwa miradi muhimu ya serikali inayolenga kuboresha sekta ya elimu nchini Tanzania. Hadi sasa, ujenzi wa shule hii umegharimu takribani TZS bilioni 4.35. Shule hii imeanza kupokea wanafunzi, na tayari zaidi ya wanafunzi 100 wapo shuleni hapo wakijifunza katika mazingira bora na ya kisasa

Licha ya mafanikio haya, juhudi za ujenzi bado zinaendelea. Mabweni ya kisasa yamepangwa kujengwa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata sehemu salama za kuishi, na ukumbi wa mikutano unaendelea kujengwa kwa lengo la kuwapa wanafunzi na walimu nafasi ya kushiriki mikutano na shughuli mbalimbali za kitaaluma na kijamii. Kuimarisha Usawa wa Kijinsia …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 pamoja na barabara unganishi yenye urefu wa kilomita 2.3

Hafla hiyo ilifanyika katika mkoa wa Simiyu, ambapo Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ipo imara na imejidhatiti kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wote nchini. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Majaliwa aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi …

Soma zaidi »

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MWENDOKASI AWAMU YA NNE WAENDELEA KWA KASI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) awamu ya nne, ikiwa ni juhudi za kuboresha usafiri wa umma jijini Dar es Salaam. Awamu hii inahusisha ujenzi wa njia kuu ya mwendokasi yenye urefu wa kilometa 13.5, inayotoka …

Soma zaidi »

Ijumaa, Desemba 20, 2024, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi rasmi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara. Nyumba hizo zimejengwa katika kitongoji cha Waret, Hanang, ikiwa ni juhudi za Serikali kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika na kuimarisha ustawi wao

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapa pole waathirika wote na kusisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwasaidia. “Ujenzi huu ni ishara ya upendo na kujali kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, aliyetoa maelekezo ya kujenga nyumba bora na za kudumu kwa …

Soma zaidi »

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud kufuatia mwaliko wa Rais huyo yaliyofanyika katika Ikulu ya Nchi hiyo jijini Mogandishu

Viongozi hao wameelezea kuhusu dhamira yao ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi kati ya mataifa hayo mawili. Waziri Kombo yupo nchini Somalia kwa ziara ya kikazi ambapo aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya kutia saini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Jamhuri ya …

Soma zaidi »

Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia kada ya Ununuzi na Ugavi nchini.

Mhe. Dkt. Biteko alisema kuwa Sekta ya Ununuzi na Ugavi ndio eneo pekee linalochukua takribani asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali, hivyo uadilifu pekee ndio utakaosaidia fedha kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa hasa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri …

Soma zaidi »

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni awasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Desemba 16,2024, baada ya kuteuliwa hivi karibuni

Waziri Masauni amepokelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Soma zaidi »

DKT. NCHEMBA AHIMIZA USHIRIKIANO WA KIKODI NA OMAN

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza katika kikao kifupi na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mapato ya Oman, Bw. Nasser Khamis Al-Jashmir, kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Oman na Tanzania katika eneo la kodi ili kurahisisha ufanyaji biashara kwa faida ya nchi hizo mbili. …

Soma zaidi »

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ubia wa Wadau wa Maji Kusini mwa Afrika (Global Water Partnership (Southern Africa & GWP Africa Coordination Unit), alishiriki Mkutano wa Bodi wa Taasisi hiyo uliofanyika tarehe 13 Desemba, 2024, mjini Pretoria, Afrika Kusini

Miongoni mwa masuala mengine, mkutano huo wa mwisho wa mwaka ulijadili jinsi GWPSA inaweza kuongeza ufanisi na kupanua zaidi shughuli zake za kutoa msaada wa kifedha na kitaalamu katika sekta ya maji kwa nchi nyingi zaidi barani Afrika. Kama sehemu ya mikakati ya kufikia lengo hilo, GWPSA imepanga kushirikiana kwa …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Desemba 14, 2024 ametembelea kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha CURE AFYA kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam

Akizungumza baada ya kushuhudia uzalishaji wa dawa kwenye kiwanda hicho chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 50, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanapata faida kutokana na shughuli zao. “Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye …

Soma zaidi »