DIPLOMASIA

WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika kesho Januari 15, 2025. Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO …

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo kwa njia ya mtandao katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2025

Soma zaidi »

Je, ni mikakati gani inayoweza kutekelezwa ili kuhakikisha ongezeko endelevu la thamani ya mauzo ya kahawa ya Tanzania nje ya nchi, huku ikizingatiwa changamoto za mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji fedha na ushindani wa kimataifa?

#MSLAC#Katibanasheria#SSH#CCM#KaziIendelee#Nchiyangukwanza#SisiniTanzania#matokeochanya @SuluhuSamia @matokeochanya @sisiniTanzania @KassimMajaliwa_ @dr_mpango

Soma zaidi »

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud kufuatia mwaliko wa Rais huyo yaliyofanyika katika Ikulu ya Nchi hiyo jijini Mogandishu

Viongozi hao wameelezea kuhusu dhamira yao ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi kati ya mataifa hayo mawili. Waziri Kombo yupo nchini Somalia kwa ziara ya kikazi ambapo aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya kutia saini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Jamhuri ya …

Soma zaidi »

TANZANIA NA OMANI ZASAINI MKATABA WA KUTOTOZA KODI MARA MBILI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kisultan ya Oman, zimetia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion. …

Soma zaidi »