Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu Kailima R.K, amefunga kikao cha siku mbili cha Tume na Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili kamili na ambavyo vimependekeza wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais. Kikao hicho kiliitishwa kwa lengo la kujadili na kupanga kwa pamoja ratiba ya kampeni za vyama hivyo

Kikao hicho kilichoketi Agosti 25 na 26, 2025 kilishirikisha vyama vya Civic United Front (CUF), National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha Mapinduzi (CCM), National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party (ADA-TADEA).

Vyama vingine ni Tanzania Labour Party (TLP), United Democratic Party (UDP), Madini Kilimo Nishati (MAKINI), Democratic Party (DP), Sauti ya Umma (SAU), Alliance for African Farmers Party (AAFP), Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC),Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo).

Kampeni za Uchaguzi zinatarajiwa kuanza Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025 nchini kote ambapo wagombea watakaoteuliwa na Tume watafanya kampeni za kunadi sera za vyama vyao kutafuta ridhaa ya wananchi kuwapigia kura Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi mkuu.

KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura

uchaguzi2025

tumehuruyataifayauchaguzi

UchaguziMkuu

uchaguzi

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *