Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa wito wa kitaifa wa maombi kwa ajili ya Tanzania, akiwasihi Watanzania wote kumgeukia Mungu kwa unyenyekevu na toba ili taifa lirudi katika mstari wake sahihi wa haki, maadili, umoja na heshima.
Katika ujumbe wake, alioutoa kwa sauti ya matumaini lakini pia ya majonzi, Mwabukusi amesema:
“Tuombe kwa ajili ya taifa letu. Tuombe ili turudi kwenye hali ya maadili, heshima ya haki, na utu wa Mtanzania. Hili ni taifa letu, tusikubali kuliona likipoteza mwelekeo wake. Huu ni wakati wa kuinama mbele za Mungu.”
Ameeleza kuwa taifa linapitia kipindi kigumu kiadili, kimaadili na kijamii, na hakuna suluhisho la kweli bila kurudi kwenye misingi ya haki, uwajibikaji na kumcha Mungu. Ametoa rai kwa viongozi, wananchi, taasisi na kila Mtanzania kujitathmini na kuchukua hatua ya kurekebisha mambo yanayoathiri ustawi wa taifa.
Maombi haya yanakuja wakati ambapo taifa linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazogusa haki, uchumi, familia na mshikamano wa kitaifa. Katika sauti
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+