Maktaba ya Kila Siku: July 10, 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika kutumika kuwekeza katika kuendeleza miundombinu ni vema kuhakikisha michango ya wanachama ambayo imetengwa kama kinga dhidi ya misukosuko ya kiuchumi na kijamii pamoja na kukabiliana na umaskini inabaki kuwa ya kutosha kukidhi malengo ya msingi ya uanzishwaji wake

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Amesisitiza kuwepo umakini kwenye uwekezaji wa miradi ya miundombinu kwani miradi ambayo haiwezi kutekelezeka inaweza kudhoofisha …

Soma zaidi »

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ina umeme wa kutosha hatua ambayo imechangiwa na kukamilika kwa Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme ukiwemo Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambao pekee unazalisha Megawati 2115

Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo Julai 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia katika vituo vya Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II ambapo amesema licha ya kazi kubwa inayofanywa na TANESCO yapo baadhi ya maeneo yalikua na changamoto …

Soma zaidi »