Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema Mpango wa Elimu kwa Umma Kuhusu Muungano utaendelea kutekelezwa kwa uwazi na ushirikiano mpana ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia Watanzania wote, hususan vijana.
Akizungumza Desemba 19, 2025 katika kipindi cha Asubuhi Njema kinachorushwa na ZBC, Waziri Masauni amesema Waandishi wa Habari wana nafasi kubwa katika kutoa elimu sahihi kwa jamii, ndio maana Ofisi ya Makamu wa Rais imeamua kushirikiana nao kwa karibu katika utekelezaji wa mpango huo. Katika kuimarisha juhudi hizo, Ofisi imeandaa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar, itakayofuatiwa na semina kwa Wahariri wa Bara, pamoja na makongamano mbalimbali yatakayolenga kuongeza uelewa wa masuala ya Muungano.
Ameeleza kuwa walengwa wakuu wa Mpango wa Elimu kwa Umma kuhusu Muungano ni vijana, kwa kuwa wengi wao wamezaliwa baada ya Muungano wa mwaka 1964, hivyo ni muhimu kuwajengea uelewa sahihi wa historia, misingi na faida za Muungano.
▶️ Tazama video kamili upate ufafanuzi zaidi.
👍 Like,
💬 comment na
🔔 subscribe kupata taarifa na mijadala muhimu kwa taifa.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+