Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Mpango wa Elimu kwa Umma Kuhusu Muungano utaendelea kuwa endelevu ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi wote, hususan vijana.
Akizungumza Desemba 19, 2025 katika kipindi cha Asubuhi Njema kinachorushwa na ZBC, Mhe. Masauni amesema Waandishi wa Habari wana nafasi kubwa sana katika kufikisha elimu kwa umma, jambo lililoifanya Ofisi ya Makamu wa Rais kushirikiana nao kwa karibu katika utekelezaji wa mpango huo.
Ameeleza kuwa tayari Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar imeandaliwa, ikifuatiwa na semina kwa Wahariri wa Bara, pamoja na maandalizi ya makongamano mbalimbali yatakayolenga kuimarisha uelewa wa Muungano.
Kwa mujibu wa Waziri Masauni, vijana ndio wanufaika wakubwa wa mpango huu, kwa kuwa wengi wao wamezaliwa baada ya Muungano wa mwaka 1964, hivyo wanahitaji elimu sahihi na ya kina kuhusu historia, misingi na faida za Muungano wa Tanzania.
📺 Tazama mahojiano kamili kupitia ZBC
📌 Elimu kwa Umma | Muungano | Vijana | Vyombo vya Habari
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+