Muhtasari wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni nyaraka ya kimkakati inayolenga kuelekeza juhudi za maendeleo ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 25 ijayo, hadi mwaka 2050. Dira hii imeandaliwa kwa kuzingatia muktadha wa ndani na wa kimataifa, mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia, na kimazingira.
Malengo Makuu ya Dira ya 2050 ni:-
1. Ustawi wa Jamii: Kuimarisha huduma za msingi kama afya, elimu, lishe, makazi, na usalama wa jamii kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania wote.
2. Ustawi wa Kiuchumi: Kukuza uchumi shindani na jumuishi kupitia viwanda, biashara, kilimo cha kisasa, na uwekezaji wa ndani na nje.
3. Utawala Bora: Kujenga taasisi imara, uwajibikaji, haki, na ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi.
4. Mazingira Endelevu: Kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali asilia, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda mazingira.
5. Tanzania ya Kidijitali: Kukuza teknolojia, ubunifu, na matumizi ya TEHAMA katika nyanja zote za maisha.
Misingi Inayoongoza Dira hii ni pamoja na Maadili, usawa wa kijinsia, mshikamano wa kitaifa, ubunifu, ushirikiano wa kimataifa, na maendeleo jumuishi.
Mtazamo wa 2050: Ni Tanzania iliyo na jamii iliyostawi, yenye uchumi wa viwanda na maarifa, inayoheshimu haki za binadamu, inayolinda mazingira, na yenye nafasi ya ushindani katika soko la dunia.
Dira hii imekusudiwa kuwa mwongozo wa sera, mipango ya maendeleo na bajeti kwa serikali, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa kuelekea maendeleo endelevu na jumuishi ifikapo 2050.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+