Amesema kuwa TanTrade inapaswa kufanya tafiti za uhakika na uchambuzi wa masoko ambayo bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa na kutoa taarifa hizo kwa wafanyabiashara kote nchini.

Ametoa agizo hilo (Jumapili, Julai 13, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar-es-Salaam.


“Masoko yamekuwa ya ushindani sana siku hizi, nilipotaja Soko Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) nilikuwa nataka kuwaambia kwamba leo hii tunapotaka kufanya uchambuzi wa masoko yetu, hayo ndio maeneo ya kufanya biashara, TanTrade fanyeni tafiti za uhakika na uchambuzi wa kina”
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+