
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Serikali hizo mbili katika kulinda Muungano.
Naibu Waziri Dkt. Dugange alipongeza kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Alisema kuwa kupitia maendeleo hayo yanaimarisha uchumi wa Zanzibar na ndio matunda ya Muungano.
Kwa upande wake Waziri Hamza alitoa rai kwa watendaji kutangaza zaidi fursa za zinazopatikana katika Muungano badala ya changamoto.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+