Katika operesheni maalum iliyofanyika eneo la Mlalakuwa, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Kudhibiti na Kuapmbana na Dawa za Kulevya (DCEA) wamewakamata vijana wanne wakidaiwa kutengeneza biskuti za bangi kwa ajili ya sherehe ya wanafunzi wa vyuo vikuu.
Watuhumiwa hao ni Bright A. Malisa (26), Humphrey G. Safari (26), Novatus A. Kileo (26) na Chriss P. Mandoza (26). Wakati wa upekuzi, walikutwa na biskuti 140 za bangi, puli nane na paketi tisa za bangi zenye jumla ya uzito wa kilo 2.858.
Kamishan Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo ameeleza kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana hao walikuwa wakijiandaa kusambaza biskuti hizo katika house party iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki, ikihusisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Polisi wamesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini mtandao mpana unaohusiana na utengenezaji na usambazaji wa bidhaa hizo za dawa za kulevya.
#KataaDawaZaKulevyaTimizaMalengoYako
Piga 119 kutoa taarifa
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+